Search This Blog

Friday, August 13, 2021

Mahakama ya Juu Brazil yaamuru kuchunguzwa Rais Bolsonaro

Mahakama ya Juu nchini Brazil imeanzisha uchunguzi dhidi ya rais wa nchi hiyo kwa kutuma kwenye mitandao ya kijamii nyaraka za uchunguzi wa siri wa polisi.
 
 Jaji Alexandre Moraes ameamuru kuwa Rais Jair Bolsonaro achunguzwe kwa kuziweka hadharani nyaraka ambazo zilikuwa zinahusiana na uchunguzi wa polisi juu ya kudukuliwa kwa mahakama ya uchaguzi. 
 
Udukuzi huo ulifanyika miezi kadhaa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2018, ambapo Bolsonaro anasema alizituma mtandaoni kuthibitisha hoja yake kuwa mfumo wa uchaguzi unaweza kufanyiwa ubabaishaji. 
 
Jaji Moraes amemuamuru Rais Bolsonaro kuzifuta nyaraka hizo mtandaoni na pia kuondolewa kwa afisa wa polisi aliyeongoza uchunguzi huo. Kupitia matangazo yake ya kila wiki mtandaoni, Bolsonaro amesema kuwa nyaraka hizo zinapaswa kuwapo hadharani kwa kuwa ni jambo lenye maslahi ya umma.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...