Kenya ilimaliza katika kilele cha jedwali la medali kwenye makala ya 18 ya Mashindano ya Dunia ya Vijana walio chini ya miaka 20 katika katika uwanja wa michezo wa kimataifa Moi Kasarani siku ya Jumapili.

Kenya ilijizolea jumla ya medali saba jana -dhahabu tatu, fedha na shaba tatu.

Hiyo ilifikisha idadi ya medali za Kenya kuongezeka hadi 16; dhahabu nane, fedha moja na shaba saba (8-1-7) matokeo bora kabisa nchini kwa miaka 11 kwenye kwenye mashindano hayo ya vijana duniani.

Mafanikio yao kwenye mashindano hayo yalizidi matokeo waliosajili katika ubingwa wa mwaka wa 2000 huko Santiago, 2006 mjini Beijing na 2010 huko Moncton.

Finland ilimaliza ya pili kwa medali tano -nne za dhahabu na moja ya fedha ilhali Nigeria ilimaliza ya tatu kwa medali saba -nne za dhahabu na tatuza shaa . Ethiopia ilifuata kwa medali dhahabu tatu ,fedha saba na shaba mbili .

Mkenya Benson Kiplangat ndiye aliyeifungulia Kenya msururu wa kushinda dhahabu alipompiku Muethiopia Tadese Worku katika mita 200 za mwisho ili kushinda dhahabu katika mbio za mita 5000 ili kuipa Kenya ushindi wa kwanza katika ubingwa wa mashindano hayo kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 siku ya alhamisi .

Mwenzake Kiplangat katika timu Levy Ki-bet alijishindia medali ya shaba kwa muda wa 13:26.01.

Teresiah Muthoni na Zenah Jemutai baadaye waliipa Kenya fahari Zaidi kwa kumaliza katika nafasi za kwanza na pili katika fainali ya mbio za mita 3000 na kumaliza ukame wa muda mrefu wa Kenya kushinda mbio hizo kwa upande wa vijana .

Muthoni pia aliandikisha muda wake bora wa dakika 13 na sekude 20.37 naye Jemutai akashinda medali ya Fedha kwa kumpiku Wudu .

Siku ya Ijumaa Jackline Chepkoech alitimka mapema kabla ya mzunguko mmoja kusajili ushidi wa dhahabu katika muda wake wa bora wa 9:27.40 na kuishindia Kenya dhahabu katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi huku mwenzake Faith Cherotich akishinda medali ya shaba kwa muda wa 9:44.76.

Siku ya jumamosi Kenya ilipata ushindi mwingine ambao haukutarajiwa wa medali ya dhahabu katika mashindano ya kutembea baada ya Heristone Wanyonyi kuibuka mshindi .

Amos Serem aliongeza medali za Kenya jumapili kwa kushinda mbio za mita 3000 kuruka viunzi na kurejesha kumbukumbu za za umahiri wa Ezekiel Kemboi kwenye mashindano hayo .Jana pia Emmanuel Wanyonyo aliisadia Kenya kuendeleza ubabe wake katika mbio za mita 800 alipovunja rekodi ya ubingwa wa mashindano hayo kwa wachezaji chipukizi katika siku ya mwisho ya mashindano hayo .