Search This Blog

Saturday, August 21, 2021

Kaimu rais wa zamani wa Bolivia kufunguliwa mashtaka


Ofisi ya mwendesha mashtaka nchini Bolivia imesema imefungua mashtaka ya "mauaji ya halaiki" na makosa mengine dhidi ya kaimu rais wa zamani Jeanine Anez kutokana na vifo vya waandamanaji 20 wa upinzani vilivyotokea mwaka 2019.
 
 Mwendesha Mashataka mkuu wa Bolivia Juan Lanchipa amearifu kuwa amewasilisha nyaraka za mashtaka mbele ya mahakama ya juu nchini huko ikiwemo madai kwamba Anez alihusika na mauaji ya kimbari, kosa ambalo adhabu yake inaweza kuwa kifungo cha miaka 10 hadi 20 jela. Anez, mwanasiasa wa kihafidhina aliingia madarakani mnamo Novemba 2019 baada ya mtangulzii wake Evo Morales kujiuzulu kutokana na shinikizo la wiki kadhaa ya maandamano ya umma kupinga ushindi wa muhula wa nne ambao ulikuwa ni kinyume na katiba. 
 
Mashtaka dhidi ya Anez yanahusu matukio mawili yaliyochochewa na vurugu kati ya wafuasi wa Morales, upinzani na vikosi vya usalama zilizopelekea watu 22 kupoteza maisha.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...