Na Amiri Kilagalila,Njombe
Licha ya serikali kujenga hospitali kubwa ya halmashauri ya wilaya ya Njombe huko Matembwe kwa mabilioni ya fedha za watanzania duru zinaarifu kuwapo na wastani wa wagonjwa watatu pekee kwa siku wanaokwenda kupata huduma katika hospitali hiyo kutokana na ukosefu wa vifaa tiba.
Katika ziara ya waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe. Ummy Mwalimu huko Lupembe mkoani Njombe mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Njombe dokta Suke Maghembe amesema wananchi wengi wamekuwa wakishindwa kupata huduma katika hospitali hiyo kutokana na ukosefu wa vifaa tiba jambo ambalo halileti afya katika ustawi wa jamii.
Pia dokta Maghembe ametumia fursa hiyo kumuomba waziri awasaidie kupatikana kwa vifaa hivyo pamoja na vitendea kazi vingine yakiwemo magari.
“Tunepata vifaa hii ingesaidia sana lakini pia gari ya wagonjwa”alisema Dkt Maghembe
Dokta Edward Kwetu ni mganga mfawidhi wa hospitali hiyo yeye anasema wamekuwa wakilazimika kwenda kusaidia kutoa huduma katika zahanati na kituo cha afya jirani cha Lupembe pindi wanapotokea wagonjwa katika maeneo hayo kwa kuwa wao hawana vifaa tiba katika hospitali hiyo.
“Wakati mwingine huwa tunakwenda kusaidia vituo vya jiarani hata operesheni ikitokea tunakwenda kusaidia”alisema Dokta Edward
kutokana na changamoto hizo waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa tamisemi ummy mwalimu ameahidi kupeleka vifaa tiba ili viweze kupunguza changamoto za huduma za afya kwa wananchi.
“Hospitali hii kwa siku inaona wagonjwa watatu ni matumizi mabaya ya rasilimali wakati kuna zahanti kwa siku zinaona wagonjwa mpaka mia mbili sasa hospitali ya halmashauri ambayo inatakiwa kuwa kubwa inawaona wagonjwa watatu,kwa hiyo sio matumizi mazuri ya rasilimali lakini nafahamu kwamba mganga mfawidhi anasema watu wanahitaji huduma lakini hawaji kwasababu hakuna vifaa,hilo nalibeba nawaahidi wananjombe kwamba tutalifanyia kazi”alisema Ummy Mwalimu
No comments:
Post a Comment