Search This Blog

Wednesday, August 4, 2021

Gavana wa New York ashtakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia

Rais wa Marekani Joe Biden amemtaka Gavana wa New York Andrew Cuomo ajiuzulu, baada ya kushtakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia.

"Nadhani anapaswa kujiuzulu," Joe Biden alisema katika mkutano na waandishi wa habari baada ya uchunguzi wa Mwanasheria Mkuu wa New York kuhusu madai ya unyanyasaji dhidi ya Cuomo kukamilika.

Wito kama huo pia ulitoka kwa Kiongozi wa Wengi wa Baraza la Seneti la Marekani Chuck Schumer na Spika wa Bunge Nancy Pelosi. Schumer na Pelosi pia walimtaka Cuomo ajiuzulu.

Wakili Mkuu wa New York Letitia James alisema katika ripoti ya kurasa 165 iliyotolewa asubuhi ya leo baada ya uchunguzi wa miezi minne kwamba Cuomo alitekeleza unyanyasaji wa kijinsia kwa zaidi ya mwanamke mmoja.

Gavana Cuomo alikanusha mashtaka hayo, akisema ripoti hiyo haikuonyesha ukweli wowote.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...