Search This Blog

Wednesday, August 4, 2021

Gavana Cuomo wa New York akabiliwa na shinikizo la kujiuzulu


Gavana wa jimbo la New York nchini Marekani Andrew Cuomo anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu baada ya uchunguzi kubaini aliwanyanyasa wanawake kadhaa kingono na kujaribu kumchukulia hatua mwanamke mmoja aliyemshitaki. 
 
Rais wa Marekani Joe Biden amemtaka Cuomo ajiuzulu kwa kuwa madai yaliyomkabili yamethibitishwa na matokeo ya uchunguzi.
 
 Spika wa bunge la New York, Carl Heastie wa chama cha Democratic amesema ni wazi Cuomo hawezi kuendelea kubaki madarakani na ataanzisha uchunguzi kwa lengo la kumfungulia mashitaka haraka iwezekanavyo. 
 
Cuomo ameendelea kukaidi akisema matokeo ya uchunguzi huo ni tofauti na ukweli halisi uliopo na hakuwahi kumgusa mtu yeyote kwa njia isiyofaa wala kujihusisha na vitendo visivyofaa vya kutongoza mtu kutaka ngono.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...