Search This Blog

Sunday, August 8, 2021

DAS Babati awatia moyo Wasanii,atoa maagizo kwa maafisa Utamaduni


Na John Walter-Babati
Maafisa utamaduni Halmashauri ya wilaya ya Babati na Babati Mji, wametakiwa kuwa karibu na wasanii  ili kukuza sanaa katika wilaya hiyo.

Wito huo umetolewa na Katibu tawala wilaya ya Babati Halfan Matipula wakati akizungumza na kikundi cha Sanaa ya uigizaji Magugu House of Talent katika Hotel ya White Rose Mjini Babati.

Aidha Matipula amewataka Wasanii kufanya Kazi kwa bidii bila kukata tamaa ili kupata mafanikio katika Kazi zao za sanaa.

"Kazi ya sanaa inalipa cha muhimu ni kujituma bila kuchoka,tujifunze kwa waliofanikiwa hawakukata tamaa" alisema Matipula 

Ikumbukwe kuwa Kikundi cha Sanaa cha Magugu House of Talent (MHT) agosti 8 2021 walipanga kuzindua filamu yao iendayo kwa jina la "Mama mdogo" lakini imeahirishwa.

Uongozi wa MHT umesema wameamua kuahirisha kwa sababu ambazo zimeshindwa kuzuilika hivyo watapanga tarehe nyingine kwa ajili ya uzinduzi huo.





 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...