|
Na Ezekiel Mtonyole, Arusha. Chuo cha ufundi Arusha (ATC) kupitia idara ya uhandisi wa magari kimefanikiwa kubuni na kuanza kutengeneza ndege aina ya Helkopta kupitia wataalamu wa ndani ya chuo hicho. Vile vile Chuo hicho kimefanikiwa kutengeneza baiskeli ya miguu mitatu inayotumia nishati ya jua(Solar) kwa ajili ya matumizi ya watu wenye ulemavu wa miguu itakayo wasaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kutegemea usaidizi. Akizungumza na waandishi wa habari walipofika chuo hapa kwa ziara ya kutembelea miradi iliyochini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mkufunzi wa uhandisi katika Chuo cha Ufundi Arusha Mhandisi Abdi Mjema, amesema ubunifu huo ulianza mda mrefu lakini baada ya Serikali kuwekeza mitambo ya kisasa katika Chuo hicho wanaamini kazi sasa itakuwa raisi kumaliza sehemu iliyobaki. “Kimsingi kazi hii ilianza mda mrefu lakini shida ni kwamba tulikuwa hatuna vifaa vizuri lakini sasa Serikali imewekeza katika mitambo ya kisasa inayotuwezesha kufanya kazi kwa urahisi naamini kazi hii tutaikamilisha kiurahisi sana” amesema Mjema. Amesema kwa kiasi kikubwa vifaa vinavyotumika katika utengenezaji wa ndege hiyo vinatoka hapa hapa ndani ya nchi kwenye maduka ya vifaa vya ujenzi isipokuwa injini yake ndio pekee imetoa nje ya nchi kwa kuwa hakuna kiwanda cha kutengeneza kifaa hicho hapa nchini. “Teknolojia sio uchawi bali ni ubunifu katika teknolojia na sisi tukaamua kufanya hivyo kwa kuwa utaalamu tunao, na tunaona kuna matukio mengi yanatokea hapa nchini ambapo tungekuwa na ndege ya aina hii ingetusaidia na kuepuka kuagiza kutoka nje ya nchi” amesema. Amesema Chuo hicho kipo katika hatua za awali katika kufanya utafiti ili kuweza kuanza kutengeneza ijini ya ngege hapa hapa nchini na kuepuka kuagiza nje ya nchi ambapo imekuwa ikichukua mda mrefu mpaka kufika hapa nchini. “Kwa uwekezaji huu wa serikali katika mitambi ya kisasa na ukizingatia tunawataalamu ya injini za magari tunafanya utafiti kuweza kubadilisha injini ya gari tukabadilisha ikawa injini ya ndege naamini tutafanikiwa tu” amesema. Kwa upande wake Mhandisi wa magari katika Chuo hicho Mhandisi David Raymond amesema maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yamewagusa kwa kiasi kikubwa kwani wameweza kupata vifaa vya kisasa na wanafunzi wanasoma kwa urahisi na wengi wamekuwa wakielewa kutokana na kusoma kwa vitendo. Amesema kwa sasa wameweza kutengeneza baiskeli pamoja na Helcopta na wapo mbioni kutengeza gari ambalo litatumia umeme kutokana na kupatiwa vifaa vya kisasa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.. “Tumetengeza baiskeli yenye kutumia umeme wa jua na tuna tunaendelea na utengenezaji wa Helcolta kwa hivi ni vitu ambavyo tumetengeneza kwa sasa lakini tupo mbioni kutengeneza gari kabisa litatumia umeme, vyote vinatengenezwa hapa katika idara yetu”amesema Mhandisi Raymond. Aidha,Mhandishi huyo amesema chuo hicho kinafundisha ufundi wa umeme wa magari na magari yenyewe ambapo amedai kuna madhara makubwa kupeleka magari kwa mafundi wa mtaani kwani wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa kubahatisha. |
|||
|
|
|||

No comments:
Post a Comment