Search This Blog

Wednesday, August 25, 2021

Algeria yavunja uhusiano wake na Morocco


Algeria imevunja rasmi uhusiano wake wa kidiplomasia na Morocco, wakati waziri wake wa mambo ya nje akisema hatua hiyo imetokana na mfululizo wa vitendo vya uhasama vya Morocco. 
 
Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Ramtane Lamamra katika mkutano na waandishi habari, amesema nchi hiyo imeamua kuanzia leo kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Morocco. 
 
Tangazo hilo linakuja wiki moja baada ya Rais Abdelmadjid Tebboune kuuambia mkutano wa baraza kuu la usalama la Algeria kuwa vitendo vya uhasama vya Morocco vimeilazimu nchi hiyo kufikiria upya juu ya uhusiano wake na jirani yake.
 
 Nchi hizo za kaskazini mwa Afrika zimekuwa zikivutana kwa muda mrefu. Morocco haijatoa tamko lolote juu ya uamuzi wa Algeria kutangaza kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na taifa hilo. 
 
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za kiarabu Ahmed Abdul Gheit amezihimiza nchi hizo mbili kuepuka mgogoro zaidi. Abdul Gheit ameonyesha matumaini kuwa Morocco na Algeria zitadumisha uhusiano ili kuhakikisha utulivu ndani na nje ya nchi zao.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...