Search This Blog

Thursday, July 8, 2021

Yanga yapigwa faini ya milioni 3


 Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) imeitoza Timu ya Young Africans SC faini ya sh. 3,000,000 (milioni tatu) kwa makosa yafuatayo:-

Kutumia mageti ya uwanja wa Uhuru kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu

 Kutumia mlango wa chumba cha waandishi wa habari (media center) badala ya mlango maalum unaotumiwa na timu

Kuingia uwanjani kupasha misuli (warm up) kwa kutumia mlango (Gate B) ambao haukupangwa kutumika kwa namna yoyote

Kutumia chumba cha wafanya usafi wa uwanja kwa ajili ya kubadilisha nguo badala ya chumba maalum cha kubadilishia nguo (Dressing Room).

Pia timu ya Young Africans SC inatakiwa kulipa Tsh. 850,0001= ikiwa ni gharama ya ukarabati wa mageti yaliyovunjwa wakati wa wakiingia uwanjani pamoja na makufuli ya uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyoharibiwa katika tukio hilo

Matukio hayo yalitokea katika mchezo wa Watani wa Jadi uliochezwa Julai 3, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na Kumalizika kwa Yanga kuibuka na Alama 3 kufuatia Ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Simba Sc.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...