Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema kwamba kupungua kwa kesi za maambukizi ya corona (Covid-19) ndani ya wiki 10 huko Ulaya kumefikia tamati, na wimbi jipya la magonjwa litaibuka ikiwa nidhamu haitazingatiwa.
Mkurugenzi wa WHO barani Ulaya Hans Kluge, alitoa taarifa kuhusiana na mwelekeo wa janga la corona.
Kluge alisema kupungua kwa kesi za maambukizi ya corona kwa wiki 10 Ulaya kumemalizika na kwamba kulikuwa na ongezeko la asilimia 10 kwa kesi za wiki iliyopita kutokana na kuongezeka kwa safari na kurahisishwa kwa vizuizi.
Afisa huyo wa WHO alisisitiza kwamba ikiwa nidhamu dhidi ya janga hilo barani itapuuziwa, wimbi jipya la magonjwa ya kuambukiza litaibuka.

No comments:
Post a Comment