Search This Blog

Thursday, July 22, 2021

Wema Sepetu atangaza kusaini dili nono

 


Muigizaji Wema Sepetu ametangaza kusaini dili nono na kampuni ya Ogelle ya nchini Nigeria.

Mkataba huo unahusu uigizaji kwenye filamu iitwayo “Bodies of Influence” ambayo inaandaliwa nje ya Tanzania na @wemasepetu atawakilisha wasanii kutoka Afrika mashariki, pia watakuwepo waigizaji wengine wakubwa wanne kutoka nchi nyingine nne za Afrika kwenye filamu hiyo.

Ogelle ni kampuni ambayo inaandaa na kuonyesha filamu kupitia Application (App) iitwayo Ogelle, pia ni jukwaa ambalo mtayarishaji wa filamu au video za muziki anaweza kufungua akaunti akaweka kazi zake kama njia ya kujipatia mapato.

Kwasasa App ya Ogelle inaruhusu tu kazi za sanaa kutoka mataifa ya Afrika.

Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari, Janet Mwansuka ambaye ni kiongozi wa Kampuni ya Ogelle amebainisha kuwa kampuni hii kwa sasa ina ofisi Nigeria na Rwanda na pia watakuja Tanzania.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...