Search This Blog

Monday, July 5, 2021

Waziri Mkuu wa Luxemburg alazwa hospitalini baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona


Waziri Mkuu wa Luxemburg Xavier Bettel, alilazwa hospitalini (jana) kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya corona (Kovid-19).

Ilitangazwa kuwa Waziri Mkuu wa Luxemburg, Xavier Bettel, ambaye vipimo vyake vya Kovid-19 vilichukuliwa wiki iliyopita, alikuwa amelazwa hospitalini kama hatua ya tahadhari na atahifadhiwa kwa masaa 24.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Luxemburg ilitangaza kuwa baadhi ya vipimo vitafanywa juu ya hali ya Bettel mwenye umri wa miaka 48, na kulingana na uamuzi wa madaktari, itaamuliwa iwapo Waziri Mkuu ataendelea kukaa hospitalini.

Ilitangazwa mnamo Juni 27 kwamba Bettel alishikwa na Kovid-19, na kwamba alionyesha dalili za ugonjwa kama homa na maumivu ya kichwa. Waziri Mkuu wa Luxemburg alihudhuria Mkutano wa Viongozi wa EU mnamo 24-25 Juni, ingawa ilibainika kwamba hakuwa akijumuika sana na viongozi wengine.

Bettel alipewa dozi ya kwanza ya chanjo ya AstraZeneca ya Covid-19 mnamo Mei 6, na alikuwa amefanya miadi kwa ajili ya dozi ya pili mnamo Julai 1 kabla ya kuugua.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...