Na Thabit Madai,Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Mohammed Abdalla, amewataka wasimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha huduma za kurekebisha watoto kumaliza ujenzi huo kwa mujibu wa makubaliano yaliyokuwepo hivi sasa ili lengo la mradi huo liweze kufikiwa.
Waziri Masoud aliyasema hayo, alipokuwa akizungumza na maasifa na wapiganaji wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha huduma za kurekebisha watoto kilichopo Hanyegwa Mchana wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja.
Alisema makubaliano yaliyokuwepo hivi sasa mradi huo ni kumalizika mnamo Septemba mwaka huu ikiwemo kukamilika kwa vitu vyote vitakavyotumika katika mkataba wao huku akiwasisitiza ukamilishaji huo kuendana na thamani hasili ya fedha zitakazotumika.
Aliema, dhamira ya kujengwa kwa kituo hicho ni kupunguza msongamano uliokuwepo kwa sasa hasa watoto ambao wamekuwa wakichanganyika na wanafunzi wakubwa.
Aidha alisema kuwa pia chuo hicho mara baada ya kumalizika kitatumika kwa wanafunzi wakubwa ambapo wanatumia vifungo vya muda mfupi na wanafunzi wenye mahitaji maalum.
“Wakati natembelea mwanzo niliona mradi huu upo chini ya asilimia 50 na lakini kwa sababu ya msisitizo tuliouweka na kusimamiana kwa dhati leo hii mradi huu upo kwa asilimia zaidi ya 90 umekamilika kilichobakia ni uingizaji wa vifaa” alisema.
Sambamba na hayo, alifahamisha kuwa chuo hicho mara baada ya kumalizika kitakuwa ni cha kisasa kwa wakati huo, ambapo kitakuwa kinaendana na vyuo vya mafunzo vyengine.
Aisha alisema kuwa wanafunzi watakaopelekwa katika Chuo hicho, wanafunzi watajifunza stadi za maisha kwa utaratibu mzuri pamoja na maoneo yao watakayotumia vitakuwa na mazingira mazuri tofauti na baadhi ya vyuo vyengine.
Hivyo, aliwasisitiza wasimamizi wa ujenzi huo kuzingatia makubaliano hayo na kuwa ya kweli ili lengo lifikiwe na liweze kuanza kazi.
Nae, Kamishna wa Chuo cha Mfunzo hayo,aliahidi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na waziri na kusema kuwa watayatekeleza kwa mnuda uliopangwa na endapo kutakuwa na changamoto watazipeleka wizarani ili kuweza kufikiwa lengo lilowekwa.
“Tutatekeleza maagizo yaliyotolewa na serikali kuptia waziri wetu ili mwenzi septemba Mungu akitujaalia tutafungua Chuo hichi kama ilivyopangwa” alisema.
Aidha alisema kuwa Chuo hicho, limetengenezwa kwa ajili ya watoto ambapo kutokana na namba wanayopekea,chuo hicho ni kikubwa, hivyo, aliomba serikali kubadili matumizi ya kutumia watoto peke yao na watumie watu wengine,
Mradi huo umeanza mwaka 2016 ambapo ulitarajiwa kumalizika mwaka 2020 ambapo hadi sasa umekamilika kwa asilimia 98 ambapo umebaki masuala madogo madogo ili kuweza kufanya kazi.

No comments:
Post a Comment