Search This Blog

Sunday, July 4, 2021

Watu 2 wafariki katika mmomonyoko wa ardhi Japan

 


Watu wawili wamethibitishwa kufariki na wengine 10 kuokolewa kufuatia maporomoko ya ardhi na mafuriko yaliyoharibu nyumba na kusomba baadhi ya magari katika mji wa Atami nchini Japan. 

Kulingana na afisa wa serikali wa eneo hilo watu wengine 20 bado hawajulikani walipo. Aidha afisa wa mji wa Shizuoka ameliambia shirika la habari la AFP kuwa shughuli za uokoaji zitaanza kwa kutuma jumla ya waokoaji 1000 pamoja na vikosi 140. 

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga siku ya Jumamosi aliwatahadharisha wakaazi kuwa makini juu ya maporomoko ya ardhi yanayosababishwa na mvua. 

Kulingana na chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali NHK, mji huo ulioko takriban kilomita 90 kusini magharibi mwa Tokyo ulishuhudia mvua ya kiwango cha milimita 313 katika kipindi cha saa 48 siku ya Jumamosi. 

Hicho ni kiwango cha juu kuliko kilichoshuhudiwa katika mwezi mzima cha milimita 242.5.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...