Search This Blog

Friday, July 9, 2021

Watu 2 raia wa Haiti na Marekani wakamatwa kuhusiana na mauaji ya Rais Moise


Maafisa nchini Haiti wanasema watu wawili wanaoaminika kuwa wenye uraia wa Haiti na Marekani wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya rais wa nchi hiyo. Mmoja wa watu hao anaripotiwa kuwa alikuwa mlinzi katika ubalozi wa Canada mjini Port au Prince. 

Watu hao James Solages na Joseph Vincent ni miongoni mwa watu 17 ambao wametiwa nguvuni kufuatia kuuwawa kwa Rais Jovenel Moise na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki nyumbani kwake hapo juzi alfajiri. 

Mkuu wa polisi ya Haiti Leon Charles, kati ya hao washukiwa 17, 15 wanatokea Colombia. Charles ameongeza kwamba washukiwa wengine watatu wameuwawa na polisi huku wengine wanane wakitoroka.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...