Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua nchini India imefika watu 124.
Vifo hivyo vinatokea wakati shughuli ya uokoaji ikiendelea kutafuta dazeni ya watu wengine waliopotea.
Eneo la pwani ya magharibi mwa India imeshuhudia mvua kubwa tangu siku ya Alhamisi, huku idara ya hali ya hewa ikionya juu ya kuongezeka kwa mvua zaidi katika muda wa siku chache zijazo.
Katika jimbo la Maharasthra, watu 114 wamekufa ikiwemo wengine zaidi ya 40 waliokufa kutokana na mafuriko yaliyotokea kwenye kijiji cha Taliye, kusini mwa mji wa Mumbai.
Waokoaji wanaendelea kutafuta watu wengine 99 ambao hawajulikani waliko.

No comments:
Post a Comment