Search This Blog

Monday, July 5, 2021

Watoto wachanga na wauguzi watekwa nyara Nigeria


Vikosi vya Nigeria vimeingilia kati katika juhudi za kuwasaka waathiriwaImage caption: Vikosi vya Nigeria vimeingilia kati katika juhudi za kuwasaka waathiriwa

Watu wenye silaha nchini wamewateka nyara watoto wachanga, wauguzi na walinzi wa usalama katika hospitali iliyopo kaskazini magharibi mwa Nigeria, polisi imesema.

Idadi Kamili ya wale waliotekwa katika mji wa Zaria haijulikani.

Majambazi wa eneo hilo walifanya mashambulio ya mfulurizo kwenye kituo cha polisi na kituo cha taifa cha kifua kikuu na ukoma, kabla ya kutorokea msituni.

Afisa wa serikali katika eneo hilo amesema jeshi limeanza juhudi za kuwatafuta waathiriwa.

Takriban watu saba waliuawa katika shambulio kama hilo lililotekelezwa na watu wenye silaha mwishoni mwa juma katika jimbo la Kaduna.

Utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi ni wa mara kwa mara nchini Nigeria.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...