Search This Blog

Monday, July 12, 2021

Wananchi wa Cuba waandamana kupinga serikali


Mamia ya watu katika nchi ya Caribbean ya Cuba walipinga serikali, wakidai uhuru na kuongezeka kwashida za kiuchumi.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani, mamia ya watu waliingia barabarani katika mji wa San Antonio de los Banos, ambao uko kilomita 33 kutoka mji mkuu wa Havana, na katika maeneo tofauti ya nchi, wakipinga serikali.

Waandamanaji walimkosoa Rais Miguel Diaz-Canel kwa kutoa kauli mbiu zilizosema "Hatutaki udikteta" na "Tunataka uhuru".

Katika picha zilizoonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii, waandamanaji walidhihirisha hisia zao kali kwa ujumbe wa "Uhuru, hatuogopi", na katika mikoa mengine kuliripotiwa kuzuka kwa visa vya uporaji.

Akiwahutubia watu kwenye televisheni ya Cuba na redio ya kitaifa, Rais Diaz Canel aliwataka wananchi walinde mapinduzi ya Cuba na kusema, "Hatutasalimisha uhuru wa nchi yetu, tunatoa wito kwa wanamapinduzi wote kuingia barabarani kutetea mapinduzi. kila mahali."

Diaz-Canel alishutumu utawala wa Marekani (USA) kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu wa kisiasa nchini wakati wa aina mpya ya janga la corana (Kovid-19) na kuvuruga uchumi kwa kutumia kizuizi.

Diaz-Canel alikiri kwamba kumekuwa na uhaba wa dawa na umeme nchini kutokana na janga la corona linaloongezeka kwa kasi, na akasema kuwa itakuwa sahihi zaidi kukaa nyumbani kwa hali ya sasa.

Nchi ya Cuba, ambayo uchumi wake umedorora baada ya janga, watu wanakabiliwa na uhaba wa dawa na upatikanaji wa mahitaji ya kimsingi.

Mashuhuda wa matukio wanasema kwamba maandamano makubwa zaidi nchini humo yaliwahi kutokea Agosti 1994.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...