Search This Blog

Saturday, July 17, 2021

Wamiliki Vituo Vya Kulelea Watoto Arusha Wapewa Miezi Mitano Kujisajili

 


ZAIDI ya nusu ya idadi ya vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Arusha havijasajiliwa na vinajiendesha kiholela.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amesema vituo 36 sawa na asilimia 40.5 ya vituo 89 ndio vina kidhi matakwa ya kisheria ya kutoa huduma.


Ametoa miezi mitano kwa wamiliki wote wa vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kuwa na leseni za kutolea huduma hiyo. “Ifikapo Desemba 2021, kila kituo mkoani hapa kinapaswa kuwa kimesajiliwa na kinajiendesha kwa mujibu wa kanuni na taratibu za nchi,” alisema wakati wa kikao na wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu jijini Arusha.


Kihamia alisisitiza kuwa baadhi ya vituo havielewi kanuni na taratibu za kuzingatia katika kuwahudumia watoto.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...