Karibu watu 80wamefariki na mamia ya wengine wakikadiria hasara nchini Ujerumani kufuatia mafuriko mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miaongo kadhaa.
Mvua kubwa iliyonyesha magharibi mwa Ulaya imesababisha mito kuvunja kingo zake na kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo hilo.
Ubelgiji pia imeripoti vifo vya watu 12 kufuatia mafuriko hayo ambayo viongozi wa kisiasa wanasema yamesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Kansela wa Ujerumnai Angela Merkel ameahidi kuwasaidia kikamilifu wahanga wa mafuriko hayo
Majimbo ya Rhineland-Palatinate naRhine-Westphalia Kaskazini nchini Ujerumani yameathiriwa vibaya na mafuriko hayo.

No comments:
Post a Comment