BERLIN,Kumekuwa na mgawanyika mkali kwa wanasiasa nchini Ujerumani iliotokana na onyo la kiongozi wa wafanyikazi katika ofisi ya Kansela wa Ujerumani, ambae amenukuliwa akisema vizuizi kwa watu wasiochanja vinaweza kuwa muhimu kama viwango vya maambukizi ya virusi vya corona vitakuwa na ongezeko kubwa jipya katika miezi ijayo.
Mkuu huyo, Helge Braun aliliambia gazeti la kila Jumapili la hapa Ujerumani la Bild am Sonntag kwamba, hataraji vizuizi vyoyote vipya vinavyohusisha na makabiliano dhidi ya ongezeko la maambukizi nchini Ujerumani.
Lakini akaenda umbali wa kusema watu wasiochanja wanaweza kuzuiwa kuingia katika maeneo kama ya migahawa, kumbi za sinema na viwanja vya michezo kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa hatari za maambukizi.
Kauli yake hiyo imeibua mijadala mikali katika siasa za Ujerumani na hata ndani ya chama Kansela Merkel cha CDU.
Mgombea wa chama hicho kwa nafasi ya ukansela ambae anatarajiwa kumrithi Merkel, Armin Laschet amesema anaipinga aina yoyote rasmi au isiyo rasmi ya kuwalazimisha watu kuchanja kwa wakati huu.
Zaidi ya asilimia 60 ya idadi jumla ya watu nchini Ujerumani imepata japo chanjo moja ya Covid-19 wakati asilimia nyingine 49 imekamilisha chanjo zote mbili.

No comments:
Post a Comment