Wafanyakazi wanne kutoka gazeti linalounga mkono demokrasia na ambalo sasa limefungwa la Apple Daily wanatarajiwa kufikishwa leo katika Mahakama ya Hong Kong wakikabiliwa na mashitaka ya kushirikiana na makundi ya kigeni chini ya sheria ya usalama wa kitaifa ambayo imeongeza hofu kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.
Mashitaka hayo ndio ya karibuni katika uchunguzi wa usalama wa kitaifa dhidi ya gazeti hilo la tajiri wa vyombo vya habari Jimmy Lai, ambalo liliacha kuchapisha baada ya mamia ya polisi kuvamia makao makuu yake mnamo Juni 17, na kukamata mali zake muhimu na akaunti za benki.
Polisi ilisema iliwashitaki watu hao wanne, akiwemo mmoja aliyekamatwa jana. Shirika la utangazaji la umma la RTHK liliwatambua watu hao wanne kuwa wafanyakazi wa lililokuwa gazeti la Apple Daily, akiwemo aliyekuwa mhariri mku, ambaye alikamatwa jana.

No comments:
Post a Comment