Search This Blog

Saturday, July 10, 2021

Umoja wa Mataifa waongeza muda wa misaada Syria


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kwa pamoja nyongeza ya muda wa kupeleka misaada ya kiutu kutoka Uturuki hadi kaskazini magharibi mwa Syria.

Nyongeza hiyo ya miezi sita itafuatiwa na miezi mingine sita baada ya makubaliano kati ya Marekani na Urusi makubaliano ambayo Umoja wa Mataifa unasema yatatoa fursa ya misaada itakayookoa maisha ya watu milioni 3.4 wanaohitaji misaada ya chakula na kiutu.

Suala la misaada kupelekwa kaskazini magharibi mwa Idlib eneo ambalo limeshikiliwa na waasi, limekuwa kipau mbele cha Rais Biden na alilizungumzia katika mkutano wake wa kilele na Rais Vladimir Putin mwezi uliopita.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...