Search This Blog

Thursday, July 1, 2021

Uingereza yatafuta maelezo kuhusu kukamatwa kwa Nnamdi Kanu


Uingereza imesema inatafuta maelezo kutoka kwa serikali ya Nigeria kuhusu mazingira ya kukamatwa kwa Nnamdi Kanu, ambaye analiongoza kundi lililopigwa marufuku linalotafuta kujitenga kusini-mashariki mwa Nigeria.

Bwana Kanu, 53, ambaye ana uraia pacha wa Uingereza na Nigeria. Anakabiliwa na mashtaka ya uhaini nchini Nigeria lakini aliikimbia nchi hiyo mwaka 2017 akiwa amepewa dhamana.

Alikamatwa tena Jumapili, kwa mujibu wa serikali ya Nigeria, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu namna alivyokamatwa na eneo alilokamatwa.

Ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria umeiambia BBC kuwa inatafuta ufafanuzi kuhusu ''uhalali'' wa kukamatwa kwa Bw. Kanu.

Umesema ulikuwa tayari kumpa "msaada wa kibalozi".

Msemaji, Dean Hurlock, amesema Bw. Kanu hakukamatwa Uingereza wala kusafirishwa kutokea huko.

Amesema kuwa Uingereza inatarajia kesi yake itafuata taratibu zinazofaa.

Bw. Kanu kwa sasa anashikiliwa na polisi wa siri baada ya mahakama ya juu kuamuru kushikiliwa kwake Jumanne.

Kesi yake inatarajiwa kuanza tarehe 26 mwezi Julai.






No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...