Search This Blog

Friday, July 30, 2021

Tunisia yatangaza waziri mpya wa mambo ya ndani


Rais wa Tunisia Kais Saied amemteua mshauri wa zamani wa usalama wa kitaifa kama waziri wa mambo ya ndani, siku chache baada ya kuchukua hatua zilizolinganishwa na wapinzani wake kuwa ni sawa na mapinduzi ya kijeshi. 
 
Mteuliwa huyo mpya, Ridha Gharsallaoui, pia aliwahi kuwa afisa wa polisi wa ngazi ya juu. Ofisi ya rais imetangaza uteuzi huo huku Saied, akiwa chini ya shinikizo la kimataifa na la kikanda la kuunda serikali mpya. 
 
Wananchi wa Tunisia wanasubiri uteuzi wa waziri mkuu mpya pamoja na miongozo mingine ya kuliokoa taifa hilo lililotumbukia kwenye mgogoro wa kisiasa. 
 
Ni muongo mmoja tangu vuguvugu la maandamano ya kudai demokrasia la mwaka 2011, na wananchi wengi wanasema hawajaona mabadiliko yoyote ya kuboresha maisha. 
 
Na wamechoshwa na mivutano ya muda mrefu kati ya wanasiasa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...