Search This Blog

Wednesday, July 14, 2021

Tume ya Umoja wa Afrika yalaani vurugu na uporaji Afrika Kusini


Tume ya Umoja wa Afrika imelaani vurugu na uporaji ulioibuka nchini Afrika Kusini kufuatia kukamatwa kwa Rais wa zamani Jacob Zuma.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Musa Faki Muhammed alitangaza kuwa wanalaani kwa nguvu zote kuongezeka kwa vurugu nchini Afrika Kusini ambazo zilisababisha vifo vya raia, uporaji wa mali ya umma na ya kibinafsi, uharibifu wa miundombinu, pamoja na kusimamishwa kwa huduma za kimsingi.

Akitoa wito wa kurejeshwa kwa amani na utulivu nchini haraka iwezekanavyo kwa heshima kamili ya sheria, kiongozi alisema,

"Kushindwa kufanya hivyo kunaweza kuwa na athari kubwa sio kwa nchi tu, bali kwa kanda nzima."

Maandamano ambayo yalianza tarehe 9 Julai kutaka msamaha wa Rais wa zamani Zuma, ambaye alihukumiwa kifungo cha miezi 15 gerezani, yalibadilika kuwa ghasia na vurugu kali.

Kutokana na hali ya vurugu nchini humo, watu 72 wamepoteza maisha hadi kufikia sasa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...