Nyota wa Manchester City na England Raheem Sterling yuko tayari kusikiliza ofa ya kuondoka klabuni hapo. Lakini meneja Pep Guardiola anataka winga huyo mwenye umri wa miaka 26 kubakia Etihad, licha ya Real Madrid kuonyesha kumuhitaji (Athletic).
Gareth Bale, 31, anaweza kustaafu kucheza soka la klabu mara baada ya mkataba wake mnono na Real Madrid anaolipwa £600,000 kwa wiki utakapokoma msimu ujao. Kumekuwa na tetesi nyingi tangu kurejea kwa mshambuliaji huyo wa Wales aliyekuwa anacheza kwa mkopo Tottenham. (Mail)
Crystal Palace imeanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, muingereza Morgan Rogers, 18. Kocha mpya wa klabu hiyo Patrick Vieira anataka kuboresha na kuweka sawa uwiano wa umri katika kiosi hicho msimu huu. (Mail)
Kiungo wa England Kalvin Phillips, 25, ana furaha kwenye klabu yake ya Leeds United na hana mpango wa kuikacha klabu hiyo ya Elland Road, kwa mujibu wa wakala wake. (The i newspaper)
Klabu za Chelsea na Arsenal zinamfuatilia mlinzi wa Bayer Leverkusen na Burkina Faso Edmond Tapsoba. Lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 amewaambia waandishi wa habari kwamba 'hakuna ofa ya uhakika na rasmi' iliyowasilishwa kwake, kwa maana hiyo ataendelea kuwa na wajerumani hao msimu mpya utakapoanza. (Metro)
Aston Villa inaamini kwamba inaweza kumpata kiungo wa Arsenal Emile Smith Rowe na watawasilisha dau jingine la tatu kwa ajili ya muingereza huyo. (Football Insider)
Arsenal inaendelea kumshawishi mlinzi wa Brighton Ben White, 23, ambapo tayari imeshawasilisha dau la £50m kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England. Hata hivyo inaelezwa kwamba dau hilo halijakubalika kama inavyoripotiwa na vyombo vingi vya habari. (Argus)
Southampton wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa mkopo wa mlinzi wa Manchester United Brandon Williams. Saints walimtaka kinda hilo la kiingereza lenye umri wa miaka 20 tangu msimu uliopita, lakini United hawakutaka kumruhusu kuondoka. (Mail)
Burnley imeonyesha nia ya kumtaka Wayne Hennessey, aliye huru. Mlinda mlango huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 34 anatakiwa pia na vilabu vya Chelsea na Aston Villa baada ya kuondoka Crystal Palace mwezi uliopita kufuatia kumalizika kwa mkataba wake. (Mail)
Barcelona itawapa nafasi Chelsea ya kumsajili mshambuliaji wake Antoine Griezmann. Magwiji hao wa Catalan wanaokabiliwa na tatizo la kifedha wanataka kumpiga bei mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 30 ili kukamilisha mkataba mpya wa Lionel Messi. (Star)
Hata hivyo Rais wa Barcelona Joan Laporta anasema "kila kitu kinakwenda sawa", licha ya mkataba huo wa Messi, 34, kumalizika na kumfanya kwa mchezaji huru. (Marca)
Manchester United na Arsenal wanataka kumsajili mlinzi wa kati wa Barcelona Samuel Umtiti. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 27 anaonekana kutokwenda sawa na mipango ya meneja Ronald Koeman. (Star)

No comments:
Post a Comment