Wanamgambo wa Taliban wamesema kuwa wamechukua udhibiti wa asilimia 85 ya Afghanistan baada ya kuziteka njia muhimu za mpakani katika mpaka wa nchi hiyo, Iran na Turkmenistan.
Hii ni sehemu ya kampeni inayofanywa na kundi hilo wakati ambapo majeshi ya Marekani yanaondoka katika nchi hiyo iliyozongwa na vita. Haya yamefanyika saa chache baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuutetea uamuzi wa Marekani kuyaondoa majeshi yake nchini humo.
Serikali ya Afghanistan imekuwa ikipuuzilia mbali madai hayo ya Taliban ya utekaji wa maeneo ikisema hatua hiyo haileti tija yoyote ila kutekwa kwa njia kadhaa za kuingia nchini humo mpakani na maeneo kadhaa yaliyo na utajiri wa madini inamaanisha kwamba hazina za kundi hilo zitakuwa na vyanzo kadhaa vya mapato.

No comments:
Post a Comment