Search This Blog

Saturday, July 24, 2021

TAKUKURU Pwani yatoa tahadhari nzito dhidi ya matapeli


NA VICTOR MASANGU,PWANI 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Pwani imewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya matapeli wanaojifanya ni maofisa wa Taasisi hiyo ili waweze kuchukuliana hatua Kali za kisheria.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzana Raymond ametoa  tahadhari hiyo akitoa taarifa ya utendaji kazi wa miezi mitatu kwa waandishi wa habari

Suzana alisema wapo wanachi wamekuwa wakipigiwa simu na watu wanaodaiwa kuwa ni matapeli wakitakiwa kufika kwenye ofisi za TAKUKURU na wanapofika hapo hakuna taarifa za wito wao.

Aidha Suzana ameongeza kuwa  katika kipindi cha miezi mitatu kutoka April hadi June  wamepokea malalamiko 127 kati ya hayo 57 uchunguzi wake unaendelea na  70 hayahusiani na Taasisi hiyo.

Alisema katika kipindi hicho kesi 15 ziliendelea  kuendeshwa katika mahakama mbalimbali za mkoa wa Pwani na kwa miezi hiyo mitatu kesi sita zilitolewa maamuzi na Jamhuri ilishinda na washitakiwa walitakiwa kulipa faini au kutumikia kifungo.

   Pia katika hatua nyingine aliwahimiza wananchi wote wa mkoa wa Pwani kuhakikisha wanawafichua watu wote ambao wanavunja Sheria kwa kujifanya wao ni watumishi wa Takukuru.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...