Search This Blog

Tuesday, July 13, 2021

Sheikh Mkuu: Sikukuu ya Eid El-Adh'haa itakuwa Julai 21


 Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir ametangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Adh'haa itakuwa Julai 21, 2021, ambapo itakuwa siku ya mapumziko kitaifa.

Taarifa ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) imeeleza kuwa maadhimisho ya sikukuu hiyo kitaifa yatafanyika mkoa wa Dar es Salaam ambapo swala itafanyika katika Msikiti wa Mtara na Baraza la Eid litafanyika hapo hapo.

Mufti ametumia nafasi hiyo kuwatakia Waislam na Watanzania wote sikukuu njema na amewaomba kusherehekea kwa usalama na amani huku wakiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO-19.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...