Search This Blog

Monday, July 26, 2021

Serikali yaipiga jeki KCMC mitungi 300 ya Oksijeni

Serikali kupitia Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) imeipatia Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC, mitungi 300 ya Oksijeni kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye changamoto ya upumuaji waliolazwa katika hospitali hiyo.

Hatua hiyo ya Serikali imekuja siku chache tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Profesa Gilleard Masenga kujitokeza hadharani na kueleza kuwa wamezidiwa na wagonjwa wanaohitaji hewa hiyo ya Oksijeni kupumua.

Profesa Masenga alisema hospitali hiyo yenye kinu cha kuzalisha Oksijeni kikiwa na uwezo wa kujaza mitungi 400 kwa saa 24, kimezidiwa kutokana na ongezeko la wagonjwa akisema mgonjwa hutumia kati ya mitungi 8 na 10 kwa siku.

Katika mahojiano yake hayo na wanahabari, Profesa Masenga alibainisha kuwa kabla ya ugonjwa wa corona kuingia nchini Machi 2020, hospitali hiyo ilikuwa ikitumia kati ya mitungi 50 hadi 60 kwa siku lakini sasa wanatumia zaidi ya 400.

Akizungumza na Mwananchi leo Julai 26, 2021, Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo aliishukuru Serikali hususan Wizara ya Afya kwa kuwapiga jeki mitungi hiyo na kufanya hospitali hiyo sasa kuwa na zaidi ya mitungi 800 ya Oksijeni.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...