Search This Blog

Wednesday, July 7, 2021

Serikali ya Afghanistan yaapa kupambana na Taliban

 


Serikali ya Afghanistan imeapa kuchukua tena udhibiti wa wilaya zote kutoka mikononi mwa kundi la Taliban wakati vikosi vya kimataifa vya usalama vikikaribia kuondoka kabisa nchini humo. 

Mshauri wa usalama wa kitaifa wa serikali ya Afghanistan Hamdullah Mohib amewaambia waandishi wa habari kuwa licha ya changamoto zilizopo, wataendelea kuwalinda raia wa nchi hiyo na kuwa wana mipango ya kuchukua tena udhibiti wa wilaya zilizoko mikononi mwa Taliban. 

Serikali imepeleka mamia ya makomando kupambana na mashambulizi ya kasi yanayofanywa na wanamgambo wa Taliban, siku moja tu baada ya wanajeshi 1,000 wa Afghanistan kukimbilia nchi jirani ya Tajikistan. 

Mapigano yameendelea kushuhudiwa katika wilaya kadhaa, lakini wanamgambo wa Taliban wameongeza kasi ya mashambulizi hasa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo na wamechukua udhibiti wa sehemu kubwa katika muda wa miezi miwili iliyopita.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...