Search This Blog

Sunday, July 18, 2021

Rais wa Ujerumani kwa wahasiriwa wa mafuriko: 'Masaibu yenu yametuvunja moyo'


Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, ametembelea jimbo la NorthRhine Westaphalia ambalo limeathirika zaidi na mafuriko na kutoa heshima kwa waliokufa katika mafuriko. 


Steinmeier alionekana ni mwenye majonzi alisema anaomboleza pamoja na waliopoteza ndugu au marafiki, na masaibu yaliyowafika familia hizo yamewavunja moyo Wajerumani. Kulingana na gazeti la Bild am Sonntag, waziri wa Fedha wa Ujerumani Olaf Scholz, pamoja na Waziri wa Uchumi Peter Altmaier, wameahidi msaada kwa wahanga wa mafuriko hayo. 


Wakati huo huo Kiongozi wa Chama cha Kijani Robert Habeck ametoa wito wa kutolewa msaada wa haraka kwa waathiriwa, amesisitiza juhudi za pamoja na za ulinzi zaidi kuwekwa ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Idadi ya vifo kutokana na mafuriko katika sehemu za mataifa ya magharibi mwa Ulaya ilipindukia 160 kufikia Jumamosi. 


Huku maji yakiendelea kupungua, wafanyakazi wa huduma za dharura wanaendelea kuondosha vifusi na kufanya jitihada za kuzuwia uharibifu zaidi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...