Search This Blog

Thursday, July 29, 2021

Rais mpya wa Peru ahaidi mabadiliko ya katiba

 


Mwanasiasa wa mrengo wa shoto Pedro Castillo ameapishwa kama rais wa tano wa Peru katika kipindi cha miaka mitatu, ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 200 ya uhuru wa taifa hilo, kwa ahadi ya kuifikisha kikomo rushwa na kulipa taifa hilo katiba mpya.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 51, aliyekuwa mwalimu wa shule wa kijijini, ameanza kazi akitaja orodha ndefu ya mambo ya kuyashughulikia kuanzia tatizo la ajira, janga la virusi vya corona, uchumi unaoyumba hadi machafuko ya kisiasa.katika hituba yake hiyo Castillo amesema Peru haiwezi kusalia mfungwa wa katiba ya 1993, kwa hivyo atapeleka muswada bungeni ili kuandaliwe kura ya maoni ya kuifanyia mabadiliko.

Kiongozi huyo kutoka chama cha Free Peru, ambae ameibuka na ushindi dhidi ya Keiko Fujimori katika uchaguzi wa marudio, hana nguvu kubwa ya viti vya ubunge, katika bunge lililogawika lenye viti 130.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...