Jeshi la Polisi limesema limejipanga vizuri kuhakikisha Usalama katika Mchezo wa Simba na Yanga utakaochezwa Julai 3 katika Uwanja wa Mkapa Dar. Hata hivyo Wazazi na Walezi wameshauriwa kutoenda na Watoto uwanjani ili kuepuka madhaara yoyote
Pia, Jeshi hilo limetaarifu kuwa watafunga Barabara ya kuelekea Uwanja wa Mkapa kutokea Keko/VETA hivyo wenye vyombo vya usafiri wanashauriwa kutumia Barabara ya Mandela na Chang’ombe
Mashabiki wameshauriwa kufika Uwanjani mapema ili kuepuka msongamano wakati wa kuingia, pia wametakiwa wasibebe vifaa vyovyote hatarishi

No comments:
Post a Comment