Search This Blog

Friday, July 2, 2021

Kenya imepitisha sheria inayoongeza tozo katika bidhaa kutoka nje

 


Kenya imepitisha sheria inayoongeza tozo katika bidhaa mbalimbali za kilimo zinazoagizwa kutoka nje ya nchi hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta kusaini muswada wa sheria ya fedha ambayo inaongeza ushuru kwa asilimia 25 kwa mayai na kiasi kama hicho kwa vitunguu vinavyoagizwa kutoka nje.

Kenya imekuwa ikiagiza kiasi kikubwa cha mayai na vitunguu kutoka nchi za Tanzania na Uganda, hivyo ongezeko hilo la ushuru huenda ikaathiri biashara kati ya nchi hizo za Afrika Mashariki.

Wakati Kenya ikiongeza ushuru kwa bidhaa za kilimo , mataifa ya Afrika yamekuwa yakihimizwa kuondoa vikwazo vya kibiashara kupitia mkataba wa biashara huru barani (AfCFTA) , ili kuongeza biashara miongoni mwao nchi hizo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...