Search This Blog

Friday, July 9, 2021

NHC yaagizwa kukamilisha machinjio ya vingunguti

 


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ameliagiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha tarehe Mosi mwezi Agosti mwaka huu machinjio ya kisasa ya Vingunguti yanaanza kufanya kazi.

Makalla ametoa agizo hilo alipotembelea machinjio hayo, yaliyopo Vingunguti mkoani Dar es salaam.

Ameagiza NHC ambayo ni Mkandarasi wa mradi huo wa machinjio ya kisasa kufanya kazi usiku na mchana ili mradi huo ukamilike.

Ujenzi wa machinjio hayo ulioanza miaka miwili iliyopita, utagharimu takribani shilingi bilioni 12 hadi kukamilika kwake.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...