Search This Blog

Sunday, July 25, 2021

Namna ya kudumisha mahusianao ya kimapenzi na mwenza wako aliye mbali nawe


Namna sahihi ya kudumisha mahusianao yako ya kimapenzi na mwenza wako

aliye mbali nawe.

Siku zote mapenzi hupaswa kupewa thamani na nafasi kubwa kwa sababu yanaleta furaha katika maisha ya binadamu. Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea mapenzi kuvunjika. Wapo baadhi ya wapenzi wanaoishi mahali tofauti na wenza wao. 

Mambo mawili yanaweza kuwa mbalimbali kama masomo na kazi.

Umbali baina ya wapenzi hufanya penzi kutetereka kama wapendanao hawatofanya kazi ya ziada  kuhakikisha wanaziba mianya  yote itakayosababisha usaliti.

Mapenzi ya mbali ni vigumu kutetereka endapo tu wapenzi watakuwa wanapendana kwa dhati na kutamani kuwa pamoja wakati wote na mmoja wapo kuamua kujitoa muhanga na kuhamia anakoishi  au kufanyia kazi mwenzake.

Hata hivyo mnaweza kudumisha mapenzi kama mtaamua kuyafuata haya:-

Mawasiliano ya mara kwa mara

Hii ni njia muhimu sana baina ya wapendanao humfanya mtu ahisi uwepo wa  mpenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Hivyo kama unae mpenzi wako aliye mbali hakikisha unawasiliana naye mara kwa mara kwa kutumi  email,sms ,kadi au simu.

Heshimu hisia zako

Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali za mapenzi ,kama huna hisia za kweli unajikuta hufurahii mapenzi hutapata raha ipasavyo.Hivyo hakikisha unamtunzia penzi lake  mpaka pale mtakapokutana hata kama uko masomoni ama kazini.

Uaminifu pekee ndiyo utakaofanya  uwasiliane nae mara kwa mara.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...