Search This Blog

Monday, July 26, 2021

Mwanamume anayeshutumiwa kwa kumshambulia rais wa Mali afariki

Mwanamume anayetuhumiwa kujaribu kumdunga kisu rais wa mpito wa Mali, Assimi Goïta, wiki iliyopita amekufa hospitalini akiwa chini ya ulinzi, serikali inasema.

Mshambuliaji huyo, ambaye hajatambuliwa, alikamatwa baada ya kushindwa kutekeleza jaribio lake, ambalo lilifanyika wakati Bwana Goïta akihudhuria sala katika msikiti.

Taarifa ya serikali ilisema afya ya mtu huyo ilikuwa imezorota akiwa chini ya ulinzi na alipelekwa hospitalini, ambako alikufa.Sababu ya kifo chake inachunguzwa .Bwana Goïta ameongoza mapinduzi mawili nchini Mali katika mwaka uliopita.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...