Search This Blog

Thursday, July 8, 2021

Museveni: Waafrika wanaweza kuunganishwa zaidi na Kiswahili


Rais wa Uganda Yoweri Museveni Uganda amewataka Waafrika kutumia lugha ya kiswahili ili kuwa na umoja barani humo.

Akizungumza katika siku ya Muungano wa Afrika ya upatanishi inayolenga kutathimini mafanikio ya muungano wa Waafrika, Bw Museveni amesema kiswahili ni ‘’lugha ambayo haiegamii upande wowote kiasi kwamba inaweza kutuunganisha, sio lugha ya kabila yoyote ile, na sio lugha ya mtu binafsi".

Katika hotuba hiyo, amesema anasikitushwa na kukosekana kwa mshikamano wa Waafrika.

Kupitia ujumbe wake wa mtandao wa Twitter, rais huyo wa Uganda aliandika : "Waafrika tayari wana mambo mengi ya kufanana au kuhusiana, hakuna sababu ya sisi kutoungana. Ni rahisi kwa Waafrika kuungana kuliko Watu wa Ulaya, lakini la kushangaza hatuchukui mwelekeo huo’’.

Bw Museveni aliendelea kusema kuwa: ‘’wakati wazungu wa Ulaya wanapoamua kukutana, wanaanza kujiuliza tunafaa kuongea lugha gani? Kiitalia?Kiingereza?, Kiholanzi?, kijerumani? Lakini katika Afrika tunaweza kutumia lugha ya kiswahili isiyoegemea upande wowote kutuunganisha , si ya kabila lolote, sio ya mtu yeyote’’.

Lugha ya kiswahili ni lugaha inayotumiwa katika nchi mbali mbali za Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya na Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

Lugha ya Kiswahili ni lugha inayoendelea kukua na kuenea.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...