Search This Blog

Friday, July 9, 2021

Michezo ya Olimpiki kufanyika bila mashabiki


Japan imewapiga marufuku mashabiki kuhudhuria michezo ya Olimpiki wakati ambapo aina mpya ya kirusi cha Delta kimesababisha mlipuko wa Covid-19 katika baadhi ya sehemu barani Asia na Afrika huku maambukizi yakiongezeka tena Ulaya na Marekani. 

Kirusi cha Delta ndicho kirusi kinachoambukiza kwa haraka zaidi tangu kuanza kwa janga la virusi vya corona mwanzoni mwa mwaka 2020. 

Awali Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga alitangaza kwamba Mji Mkuu Tokyo utawekwa katika hali ya tahadhari katika kipindi chote ambacho michezo hiyo itakapokuwa ikiendelea. 

Hatua hii ni kinyume na hali ilivyokuwa wiki iliyopita ambapo baadhi ya maafisa walikuwa wangali wakisisitiza kwamba mashabiki bado wanaweza kuhudhuria michezo hiyo. 

Michezo ya Olimpiki inaanza Julai 23 na kukamilika Agosti 8.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...