Search This Blog

Wednesday, July 21, 2021

Mhe.Gekul asisitiza COSOTA kutumia Maafisa Utamaduni kutoa Elimu kuhusu Hakimili kwa Wasanii


Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul aisisitiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuwatumia Maafisa Utamaduni wa ngazi za Mikoa, Wilaya na Halmashauri kutoa elimu ya masuala ya hakimiliki kwa wasanii na makundi mbalimbali.

Mheshimiwa Gekul ametoa msisitizo huo Julai 20, 2021 Jijini Dar es Salaam alipotembelea COSOTA  kufahamu majukumu  na mikakati yao katika kurahishisha utoaji wa huduma na ukusanyaji wa mirabaha ambapo aliwasihi kuongeza kasi katika kutoa elimu ili waweze  kukusanya vizuri.

‘’Jitahidini kuongeza kasi katika kutoa elimu kwa wadau kwa kuwatumia Maafisa Utamaduni kutoa elimu kwa wasanii na kwa nyie Maafisa wa COSOTA na gawaneni mikoa kila mmoja awe na jukumu la kuwasiliana na afisa utamaduni wa mkoa fulani kwa lengo la kusaidia kutoa elimu na kwa mambo ambayo hayajakamilika kama  marekebisho ya kanuni harakisheni kukamilisha,’’alisema Gekul.

 Naibu Waziri huyo ameipongeza COSOTA kwa namna inavyofanya kazi huku akiwasihi mara baada ya kukamilisha marekebisho ya kwa kanuni wanazofanya kuhakikisha wanawapitisha na kuwaelimisha Maafisa Utamaduni kwa lengo kuweza kuwasaidia ili muweze kukusanya kwa kasi.

Kwa upande wa Kaimu Afisa Mtendaji na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Andrew Shirima alieleza majukumu mbalimbali ya COSOTA pamoja na kufafanua kuhusu mchakato wa upatikanaji wa mfumo wa wa ukusanyaji wa mirabaha  na namna mfumo huo utakavyo kuwa unafanya kazi na kurahisisha ukusanyaji wa mapato.

‘Mwezi huu wa Julai tumesaini mkataba na TTCL kwa ajili ya mfumo waliyouandaa wa kuuza kazi mbalimbali za Sanaa ikiwemo filamu ambapo utakuwa unauza filamu kwa viwango vya kimataifa kama ilivyo Netflix na jukumu la COSOTA katika mfumo huu ni kulinda hakimiliki kwa kazi zote zitakazowekwa katika mfumo huo,’’amesema Shirima.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...