Search This Blog

Friday, July 2, 2021

Mhandisi Mfugale kuagwa Dar leo


 Mwili wa aliyekuwa  mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), mhandisi Patrick Mfugale umewasili katika viwanja vya Karimjee mkoani Dar es Salaam itakapofanyika ibada ya kutoa heshima za mwisho.

Viongozi mbalimbali wamewasili katika viwanja hivyo akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Hussein Katanga, mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, wakuu wa wilaya, watendaji wa Tanroads pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwa mujibu wa ratiba baada ya mwili wa Mfugale kuagwa utapelekwa nyumbani kwake Kimara Temboni saa 10 jioni ambapo kutakuwa na misa katika Kanisa la Mtakatifu Ritha na kesho Julai 3 itaanza safari kwenda Ifunda Mkoani Iringa kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumatatu Julai 5, 2021



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...