Search This Blog

Wednesday, July 14, 2021

Mbunge wa Babati Vijijini awataka Viongozi watatue kero za wananchi


Na John Walter-Babati

Mbunge wa Babati vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo amewataka watendaji wa vijiji,kata na wenyeviti  pamoja na viongozi wengine kutatua kero zilizo ndani ya uwezo wao na sio kusubiri viongozi wa juu wafanye ziara na kukutana nazo.

Mhe. Sillo alieza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata za Kiru na Arri ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa Jimbo hilo na kuwahimiza kufanya kazi.

Alieleza kuwa kuwepo kwa migogoro hiyo kunasababishwa na baadhi ya viogozi na watendaji wasiokuwa waaminifu kwa kutenda vitendo viovu, hivyo kuwasihi wasimamizi na viongozi hao kuacha mara moja tabia hiyo kwani serikali ya awamu ya sita inawataka wananchi wafanye kazi zao kwa uhuru hivyo haitomvumilia mtendaji yoyote atakaejihusisha na vitendo hivyo.

Alifafanua kwamba mbali na kero ya uwepo wa migogoro ya ardhi lakini pia kumekuwepo na muendelezo wa vitendo viovu vya rushwa katika upatikanaji wa haki ndani ya taasisi na katika jamii kwa ujumla.

Amesema kutatua kero za wananchi ni kumsaidia Mh Rais kwa sababu pengine ana kazi nyingi zaidi za kufanya kwaajili ya watanzania.

Kwa upande mwingine Mheshimiwa Daniel Sillo  amewataka wananchi kupelekea malalamiko yao  katika ngazi ya vijiji au mitaa kabla ya kuifikisha ngazi za juu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...