Search This Blog

Friday, July 23, 2021

Marekani yamwekea vikwazo waziri wa ulinzi wa Cuba

 


Marekani imemwekea vikwazo waziri wa ulinzi wa Cuba na kikosi maalumu cha wizara ya mambo ya ndani, kwa ukandamizaji dhidi ya maandamano ya amani. 

Rais Joe Biden wa Marekani amesema huo ni mwanzo tu wa hatua za kuiadhibu Havana. Wizara ya fedha ya Marekani imesema ofisi yake ya udhibiti wa mali za kigeni imezuia mali za waziri Alvaro Lopez Miera na kikosi maalumu cha kitaifa kutoka wizara ya mambo ya ndani ya Cuba, kuhusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa wakati wa maandamano ya amani mapema mwezi huu.

 Biden amesema Washington inafanya kazi kwa karibu na washirika wa kikanda ikiwemo jumuiya ya mataifa ya Amerika ili kuzidisha shinikizo dhidi ya utawala wa Cuba kuwaachia wafungwa wa kisiasa, kurejesha intaneti na kuruhusu Wacuba kufurahia haki zao za msingi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...