Search This Blog

Friday, July 23, 2021

Makandarasi watakaojenga chini ya kiwango watarudia kwa gharama zao wenyewe- DC Moyo


Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Hassan Moyo amesema Makandarasi watakaojenga chini ya kiwango Miradi ya Kimaendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa watarudia kwa gharama zao kwa ubora ule ule unatakiwa kutokana na thamani ya mradi husika

Moyo amesema miradi mingi imejengwa kwa viwango vinavyotakiwa ila tatizo kubwa lipo kwa Makandarasi ambao wamekuwa wakipewa Tenda za Ujenzi wa Miradi wanaichelewesha kwa makusudi na kusababisha kuchelewa kuanza kufanya kazi kwa miradi hiyo

Aliwataka watendaji wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ili kutumia Fedha za Wananchi vizuri kuendana na mradi ambao unakuwa unatekelezwa kwenye maeneo yao




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...