Na mwandishi wetu Mara.
Kutokana na kesi Namba 01,2020 ya udhalilishaji iliyokuwa inamkabili mwaandishi wa habari Samsoni Chacha baina ya Sinda Keteba Mahakama ya wilaya Tarime mkoani Mara imemhukumu kulipa shilingi milioni 30.
Chacha alikabiliwa na kesi hiyo kwa kumwandika Sinda Keteba kwenye Gazeti la habari leo la tarehe 24,06,2020 kuwa alikamatwa na shehena ya vitenke akiwa anasafirisha kwa kutumia gari lenye namba za usajili T 806 DSY kwa njia ya magendo akiwa anakwepa kodi ya serikali jambo ambalo mlalamikaji alikana kuwa si kweli.
Akisoma hukumu Hakimu wa mahakama hiyo,Veronica Selemani kwa niaba ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Veronica Mugendi aliyekuwa akiiendesha kabla ya kuhama alisema mshitakiwa anatakiwa kulipa shilingi milioni 30 na gharama za kesi pamoja na kulipa asilimia 7% ya shilingi milioni 30 alizohukumiwa kila siku tangu siku hukumu ilipotolewa.
Hakimu huyo alisema kuwa mahakama imesikiliza kesi hiyo kwa makini pamoja na ushahidi uliotolewa wa pande zote mbili mahakamani hapo na kugundua kuwa mshitakiwa Samsoni Chacha anamakosa ya kuandika habari za kumchafua mlalamikaji Sinda Keteba kwenye Gazeti.
Awali kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na kusikilizwa na Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya Veronica Mugendi kabla hajahama huku wakili wa kesi upande wa mlalamikaji akiwa DominicJeremiah Chacha.
Hakimu huyo aliongeza kusoma kuwa mshitakiwa anatakiwa kulipa shilingi milioni 30 na asilimia 7 ya shilingimgi milioni 30 iliyotolewa na mahakama kulipa tangu siku ya hukumu ilipotolewa tarehe 02,07,2021 huku Chacha akitkiwa kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi.
Hukumu hiyo ilisema kuwa kutokana na kosa la kudhalilishwa Keteba sasa jamii haina imani naye na kuwa mlalamikaji kutokana na habari hizo kampuni ya Karntin Company LTD imemsimamisha kazi ikiwemo kusimamishwa nafasi ya Ujumbe wa halmashauri ya kijiji cha Buriba.
Mhakama hiyo pia imetoa nafasi kwa mtu yeyote ambaye hakuridhika na uwamuzi wa mahakama uliotolewa kuwa anayo nafasi ya kukata rufaa katika mahakama ya juu yake yake.

No comments:
Post a Comment