Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza Ujerumani, Robert Koch jana imerekodi visa vipya 754 vya virusi vya corona na imethibitisha vifo sita.
Hata hivyo, idadi ya maambukizi mapya kwa watu 100,000 katika kipindi cha siku saba yameongezeka kwa siku ya tano mfululizo na kufikia 6.2 ikilinganishwa na 5.8 siku ya Jumamosi.
Ingawa takwimu ziko chini, maambukizi yameongezeka licha ya kuwepo wasiwasi kuhusu kuenea kwa aina ya kirusi cha delta.
Aidha, maafisa wa afya wa Libya wameonya kuwa virusi vya corona vinaongezeka, ambako imerekodi visa vipya 2,854 siku ya Jumamosi, kutoka 719 wiki moja kabla.
Brazil kwa upande wake imerekodi visa vipya 48,504 na vifo 1,205. Nako Thailand, zaidi ya wafanyakazi 600 wa afya wameambukizwa COVID-19, licha ya kupata chanjo zote mbili za China za Sinovac.

No comments:
Post a Comment