Search This Blog

Friday, July 30, 2021

Kibali cha kimataifa cha kukamatwa kwa Simone Gbagbo wa Ivory Coast chafutwa


 

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC) imeondoa hati ya kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Simone Gbagbo.

Alikuwa akikabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa wakati wa mzozo wa baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010- 2011, baada ya mumewe kukataa kukabidhi madaraka kwa Alassane Ouattara, ambaye alishinda uchaguzi wa mwaka 2010.

ICC ilisema "ushahidi ambao hati ya kukamatwa kwa Simone Gbagbo ilitegemea haingeweza kuzingatiwa tena kuwa ya kutosha.

Hati hii, kwa hivyo ilionekana kuwa isiyofaa na haiwezi kutumika tena"Mnamo mwezi Machi, mahakama ilimwachilia huru Laurent Gbagbo aliyekuwa amekamatwa Kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na akarejea nchini Ivory Coast mnamo Juni 17.

Rais huyo wa zamani na Rais Ouattara walikutana kwa mara ya kwanza katika kipindi cha muongo mmoja, Jumanne.Bwana Gbagbo aliwasilisha talaka dhidi ya aliyekuwa Mke wake Simone mnamo mwezi Juni.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...